Bi Halima Begum amesema hayo baada ya Mahakama ya Juu ya Uingereza kukataa kusimamisha uuzaji wa vipuli vya ndege za kivita za F-35 kwa Israel inayotenda jina kila uchao dhidi ya Wapalestina.
Dk Halima Begum, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Oxfam, ameelezea kusikitishwa kwake na uamuzi wa mahakama ya Uingereza wa kukataa kusitisha usafirishaji wa vipuli vya ndege za kivita aina ya F-35 kwenda Israel, ambazo zinatumika katika mashambulio dhidi ya Gaza.
Begum alielezea uamuzi huo kama "wa kushangaza na wa kukatisha tamaa sana" na kusema: "Mahakama na serikali zimekubali kwamba silaha za Uingereza ziko katika hatari ya kukiuka sheria za kimataifa za kibinadamu huko Gaza, lakini zimetanguliza usambazaji wa ndege za kivita mbele ya maisha ya Wapalestina. "Haikubaliki kwamba serikali inaendelea kuidhinisha uuzaji wa vifaa vya ndege za F-35 ikijua kwamba zinatumiwa kuwalenga raia wa Gaza kwa makusudi na kuharibu suhula zao za kuishi, ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji."
Msimamo wa mkurugenzi huyo mtendaji wa OXFAM yenye makao yake makuu nchini Uingereza yamekuja baada ya Mahakama ya Juu ya Uingereza kukataa hoja ya kundi la kutetea haki za binadamu liitwalo Al-Haq mwezi uliopita. Kuundi hilo lilikuwa limesema kuwa, uamuzi wa kuipa serikali ya Uingereza kibali cha kupeleka vifaa na suhula za andege za kijeshi kwa Israel ni kinyume cha sheria na ulikiuka wajibu wa nchi hiyo chini ya sheria za kimataifa.
342/
Your Comment